Kijana Aliyedungwa Na Samaki Shingoni Hadi Kutokea Upande Wa Pili Asimulia Ilivyokuwa

Muhammad sehemu ilipomdunga samaki
Kijana wa Indonesia ameelezea kile alichokumbana nacho kwa mara ya kwanza wakati alipokuwa anaogelea na ghafla akaona samaki ametoka majini, akamrukia na kumdunga shingoni.
Muhammad Idul ameelezea vile samaki aina ya ngarara alivyoruka kutoka majini na kumdunga kwenye shingo yake, na kulazimika kuogelea kwa hara kuelekea ufuoni kabla ya kukimbizwa hospitalini dakika 90 kwa gari.
Kijana huyo wa miaka 16 kuwa hai, na kuweza kusimulia yaliyompata imekuwa kama miujiza baada madaktari kumfanyia upasuaji.
Jeraha alilopata Muhammad limemfanya kuwa maarufu baada ya picha za samaki aliyemdunga shingoni kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kote ulimwenguni.
Akizungumza BBC Indonesia, siku tano ya kutokea kwa tukio hilo, anasema kwamba walikuwa wamepanga kuvua samaki usiku akiwa pamoja na rafiki wake wa shuleni, Sardi.
"Mashua ya Sardi ilitangulia na mimi nikamfuata kwa kutumia mashua nyengine," anakumbuka kilichotokea. "Takriban mita 500 kutoka ufuo wa bahari, Sardi akawasha taa.
"Samaka aina ya ngarara aliruka kutoka kwenye maji na kuniuma shingo yangu."
Hapo hapo, Muhammad alianguka kando ya mashua giza likiwa limetanda kila sehemu. Samaki huyo mrefu, mwembamba na mwenye taya kali akamuuma shingoni, chini tu ya kidevu hadi kwenye fuvu lake.
Hata baada ya kumdunga, samaki huyo alikuwa bado anamyumbisha kijana huyo majini wakati akijaribu kutoroka.
Muhammad alimshika samaki huyo kwa nguvu akitumai kwamba hata fanya maafa zaidi katika jeraha alilopata.
"Nilimuomba Sardi usaidizi - na yeye akanishauri nisijaribu kumtoa samaki kwasababu ningetoa damu nyingi," amesema.
Hatimaye vijana hao walifanikiwa kuogelea hadi ufuoni huku Muhammad akiwa ameshikilia samaki huyo ambaye bado amekita pale alipomdunga shingoni.
Babake Muhammad Saharuddin alimkimbiza hospitalini Bau-bau, karibia saa moja na nusu kutoka kijijini kwao kusini mwa Buton, eneo la kusini mashariki mwa Sulawesi.
Baada ya kufika hospitalini, madaktari walifanikiwa kukata mwili wa samaki lakini wakashindwa kutoa mdomo wake uliodunga shingoni kwasababu ya ukosefu wa vifaa stahiki.
FNa hivyo basi wakahitajika kusafiri hadi hospitali ya mkoa iliyopo Makassar, mji wa kusini mwa Sulawesi.
Hata katika hospitali kubwa ya Wahidin Sudirohusodo, wafanyakazi walishikwa na bumbuazi baada ya kumuona mwathirika.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Khali Saleh alisema kwamba kilikuwa ni kisa cha kwanza cha aina hiyo, na walihitaji wataalam watano ili kuondoa samaki aliyesalia kwa makini kwenye upasuaji uliochukua saa moja.
Muhammad Idul
Siku 5 baadaye, Muhammad amefungwa bendeji na hana maumivu. Ingawa hawezi kugeuza shingo yake upande wa kulia lakini anaweza kutabasamu.
Hata hivyo, itachukua muda kidogo ili kupona kabisa,
"Tunafuatilia hali yake. Huenda akatolewa hospitalini siku chache zijazo lakini hawezi kwenda kijijini sababu bado anahitaji kuonekana na madaktari," Khalid Saleh ameelezea.
Aidha, licha ya tukio hilo, bado Muhammad ana ndoto ya kuendelea kuvua.
"Ninachohitajika kufanya nikuwa mwangalifu zaidi wakati mwingine. Samaki aina ya ngarara hawawezi kuhimili mwangaza - na hiyo ndiyo sababu aliruka kutoka kwenye maji na kunidunga shingoni," amesema.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon