Lukaku Azidi Kungara Inter Milan, Kocha Afunguka

Romelu Lukaku
Mshambuliaji nyota Romelu Lukaku amefunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Italia ambao Inter Milan iliichapa Napoli.

Lukaku amefikisha mabao 14 tangu alipojiunga na Inter Milan akitokea Manchester United alikoshindwa kungara chini  ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.
Romelu Lukaku
Lukaku, mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji ameonyesha kiwango bora tangu alipotua Inter Milan kwa Pauni74 milioni Agosti, mwaka jana.

Napoli imemuweka pabaya kocha Gennaro Gattuso kwani katika mechi tatu imefungwa mbili tangu alipotwaa mikoba ya Carlo Ancelotti.

“Huu ni ushindi mgumu ambao hatukutegemea, kuifunga Napoli si kazi ndogo. Tulichukua tahadhari kubwa wakati tukijiandaa kwa mchezo huo hatua iliyotufanya tujiamini,”alisema  kocha wa Inter Milan Antonio Conte.

Gattuso alisema walifanya makosa matatu yaliyozaa mabao, lakini wataendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu na ana hakika wataimarika katika maeneo mengi.


EmoticonEmoticon