Maajuza Wa Miaka 93 Na 94 Wabakwa Na Kuuawa

Umetendeka unyama huko Wiyumiririe, sehemu inayoitwa  Mutara, Nyahururu nchini Kenya ambako ajuza mwenye umri wa miaka 93 alibakwa na kisha kuuawa .

Mwili wa  mwathiriwa  Mukami Ndumia  ulipatika uchi  ukiwa  umefurika damu yake  jumatatu asubuhi katika tukio ambalo limeshtua wenyeji.

Polisi kutoka kituo kidogo cha  Ngobit wamemkamata mshukiwa mmoja kuhusiana na tukio hilo la kikatili.

Kwingineko katika tukio kama hilo ,ajuza mwenye umri wa miaka 94 naye pia alibakwa na kisha kuuawa kwa kunyongwa katika  kijiji cha Kivaani,Kangundo nchini Kenya.

Kisa hicho cha Kangundo kimejiri wiki moja tu baada ya mwanamme mmoja katika eneo hilo kukamatwa na kufikishwa kortini kwa kufanya kitendo kisicho cha kawaida na mbwa hadi kumwua  mnyama huyo .
credits:radiojambo


EmoticonEmoticon