Mabosi Wa Barcelona Walifikiria Wazo La Leo Messi

Quique Setien and Messi
Lionel Messi amemwambia kocha mpya wa Barcelona, Quique Setien kumsajili straika Sergio Aguero.

Messi alikutana ana kwa ana na Setien baada ya kocha huyo wa zamani wa Betis kukutana na wachezaji wa timu hiyo kufuatia kutua Nou Camp kuchukua mikoba ya Ernesto Valverde wiki iliyopita.
Sergio Aguero
Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Hispania, mwanasoka huyo bora duniani amemwambia kocha wake kuhakikisha anakwenda kumsajili straika wa Manchester City, Aguero kwa sababu ndiye mtu anayefaa zaidi kuziba pengo la majeruhi Luis Suarez.

Suarez atakuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua miezi minne na Barca haikufuata ushauri wa awali wa Messi huyo wakati alipowapa tahadhari mapema ya kutokea kitu cha aina hiyo.
Sergio Aguero and Messi

Hata hivyo, wazo la Messi linawafikirisha mabosi wa Barcelona wakitazama kama kuna uwezekano wowote wa Man City kumpiga bei straika wake huyo matata kabisa kwa sasa.


EmoticonEmoticon