Katika uhusiano baina ya mume
na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu.
Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele
ya mwanamke.
Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao
kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele
ye mwanamke:
1.Hadaa na unyonyaji
1.Hadaa na unyonyaji
Baadhi ya
wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha
mapenzi.
Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa
ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu
matatizo ya kipesa na kiuchumi.
Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi
atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo
ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo.
2.Wanawake wengi
Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume.
2.Wanawake wengi
Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume.
Kuwa na uhusiano na wanawake wengi wasiokuwa na
ukomo, husababisha katika kushusha heshima yake mbele ya mkewe. Tambua kuwa
hiyo sio sifa nzuri ya kujivunia.
3.Uongo
Uongo ni miongoni mwa mambo ambayo mwanamke huchukia sana kuyaona kwa mwanaume. Kuna wanaume hodari katika kutunga na kusema uongo.
3.Uongo
Uongo ni miongoni mwa mambo ambayo mwanamke huchukia sana kuyaona kwa mwanaume. Kuna wanaume hodari katika kutunga na kusema uongo.
Lakini mwanamke akigundua kuwa unamuongopea, basi heshima na
thamani yako itakuwa imeshuka kabisa machoni mwake hata kama ataamua kuendelea
kuishi nawe.
4.Ukosefu wa heshima
Utovu wa heshima ni miongoni mwa mambo yanayoharibu uhusiano maridhawa baina ya wanandoa hata kama kutakuwa na mambo yanayowaunganisha.
4.Ukosefu wa heshima
Utovu wa heshima ni miongoni mwa mambo yanayoharibu uhusiano maridhawa baina ya wanandoa hata kama kutakuwa na mambo yanayowaunganisha.
Hivyo, ewe mwanaume mwenzangu, usiishushe haiba ya mkeo kwa
lugha chafu au kumdhalilisha. Usishushe thamani ya vitu anavyovifanya kwa ajili
yake hata kama vitakuwa vidogo.
Daima jitahidi kuwaheshimu ndugu zake kwa
sababu ukifanya kinyume na hivyo, thamani yako mbele yake itashuka, hata kama
hatakwambia.
5.Kutomuamini
Kuaminiana ni miongoni mwa mambo mazuri ambayo yakipatikana katika mapenzi ya wawili, huwasaidia kukabiliana na vikwazo na changamoto mbalimbali.
5.Kutomuamini
Kuaminiana ni miongoni mwa mambo mazuri ambayo yakipatikana katika mapenzi ya wawili, huwasaidia kukabiliana na vikwazo na changamoto mbalimbali.
Ikiwa mume ni mtu anayetilia shaka maneno na matendo ya
mke kila siku, thamani yake machoni mwa mkewe itashuka. Kuaminiana kuna
mafungamano makubwa sana na upendo na kujiamini.
Iwapo kutakuwa na ulegevu
katika jambo hilo, mahabba yao hayatakuwa maridhawa.
EmoticonEmoticon