Man United Wataka Kumrudisha Sanches Endapo Hatothibitisha Ubora Wake

Alexis Sanchez
Manchester United imemtaka Alexis Sanchez kuthibitisha ubora wake Old Trafford huku kukiwa na taarifa za klabu hiyo kutaka kumrejesha.

Mshambuliaji huyo anayelipwa mshahara wa Pauni500, 000 kwa wiki, amepelekwa kwa mkopo Inter Milan ya Italia.
Man United inasita kumpiga bei Inter Milan na klabu hiyo imepanga kumpa nafasi nyingine ili kuthibitisha ubora wake Man United.

Mchezaji huyo mwenye miaka 31, anatarajiwa kuwemo katika kikosi kitakachokwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya wa majira ya kiangazi.

Licha ya kupelekwa Inter Milan baada ya kukosa namba Man United, Sanchez anapambana na majeraha ya mguu ingawa aliingia akitokea benchi katika mchezo waliotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Cagliari mwishoni mwa wiki.

Sanchez bado anamiliki jezi namba saba Man United na amebakiza miaka miwili kabla ya mkataba wake kumalizika.

Sanchez alitua Man United Januari 2018 akibadilisha na Henrikh Mkhitaryan aliyekwenda Arsenal. 

Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alishindwa kutamba na kufunga mabao matano katika mechi 45 alizocheza.


EmoticonEmoticon