Marekani Imemuua Mkuu Wa Iran Wa Vikosi Maalum

Qasem Soleimani, Jenerali wa vikosi maalum vya Qudsi vinavyoungwa mkono na Iran, ameuawa na vikosi vya Marekani nchini Iraq.
Pentagon imethibitisha kuwa aliuawa kufuatia "amri ya rais".
Hayo yamejiri kufuatia ripoti ya mashambulio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Baghdad, ambayo ilisema watu kadhaa wameuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa "hatari na uchokozi wa kishenzi".
Katika Twitter yake Bw. Zarif aliandika: Marekani itawajibikia chochote kitakachotokana na hatua hiyo.
Twitter yake Bw. Zarif
Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Qudsi kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.
Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.
Bei ya mafuta duniani imepanda kwa asilimia nne baada ya shambulio hilo.
Source:Bbc


EmoticonEmoticon