Mashabiki Wa Man U Wavamia Nyumba Ya Makamu Mwenyekiti Wa Klabu Hiyo, Kisa Chaelezwa

Kutokana na hali ya sintofahamu katika klabu ya Manchester United kutokana na mwenedo wa klabu hiyo wa kusuasua hadi kupelekea kufanya vibaya katika michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu.
Kumekuwa na baadhi ya mashabiki wa Manchester United wakionyesha kutofurahishwa na kazi ya Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kuwa ndio chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya na ikiunganishwa na tukio la kuonyeshwa kutofanikiwa kwa usajili wa kiungo wa klabu ya Spoting ya Ureno Bruno Fernandez huku ikielezwa sababu ni yeye.Ole Gunnar
Mbali na hilo pia wakati dirisha dogo la usajili linaanza mapema mwezi huu wa januari alisikika kocha wa United Ole Gunnar akisema kuwa anahitaji kufanya usajili wa wachezaji watatu mpaka wanne lakini hadi hivi sasa dirisha hilo la usajili limebakisha siku mbili United haijafanya usajili wowote.
Baada ya yote hayo usiku wa jana Mashabiki wa United walishambulia nyumba ya Makamu mwenyekiti mtendaji wa klabu!
Mashabiki wa Man U
Taarifa inasema: Imeripotiwa Jana usiku mashabiki wapatao 20 hadi 30 walishambulia nyumba ya makamu mtendaji wa klabu ya Man Utd – Ed Woodward huko Cheshire. huku wakisikika wakisema ” Ed Woodward gona die
Man Utd wametoa Taarifa rasmi kutokana na tukio hilo: “Mashabiki kutoa maoni ni jambo moja, uharibifu wa jinai na kusudi la kuhatarisha maisha ni jambo lingine. Hakuna samahani kwa hii.”


EmoticonEmoticon