Mashabiki Wa Soka Wapo Kwenye Hatari Ya Kupata Mshtuko Wa Moyo, Chukua Tahadhari

Mashabiki wa Yanga & Simba
Mashabiki kindakindaki wa mpira wa miguu hupata msongo wa mawazo wanapokuwa wakitazama timu zao, wanaweza kujiweka hatarini kupata mshtuko wa moyo, utafiti umeeleza.
Utafiti uliofanywa Oxford ulipima mate ya mashabiki wa Brazil wakati walipoweka historia ya kushindwa walipocheza na Ujerumani kombe la dunia la mwaka 2014.
Walikuta kiasi cha homoni kiitwacho Cortisol wakati timu ya Brazil ilipopoteza kwa kuchapwa 7-1 kwenye mechi ya nusu fainali.
Germany 7 Vs Brazil 1
Hii inaweza kuwa hatari, na kuongeza maradhi ya shinikizo la damu na kusimama kwa mapigo ya moyo.
Watafiti walibaini kuwa hakuna tofauti ya msongo wa mawazo kati ya wanaume na wanawake wakati wa mchezo, ingawa wanaume wako hatarini zaidi kutokana na ''ukaribu na timu zao za mpira''.
Mashabiki
''Mashabiki ambao wameshikamana na timu yao hupata msongo wa mawazo wanapotazama mechi,'' anasema Dokta Martha Newson, mtafiti katika kituo cha utafiti kuhusu masuala ya jamii, Oxford.
''Mashabiki wa kawaida pia hupata msongo wa mawazo lakini si kwa kiasi kikubwa kama walivyo wale mashabiki wakubwa.
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni ya coertisol kunaweza kusababisha;
1.Kubana mishipa ya damu
2.Kuongeza shinikizo la damu
3.Kuharibu moyo ambao tayari umedhoofu
Ongezeko la cortisol pia huweza kuwapa watu hisia kama vile maisha yao yako hatarini au wako hatarini kushambuliwa.
Mashabiki wa Yanga
Tafiti za awali zimeonesha ongezeko la maradhi ya mshtuko wa moyo miongoni mwa mashabiki hasa katika siku za mechi muhimu, wanapokuwa wakiwakilisha timu au nchi.

Katika utafiti wao, watafiti wa Chuo cha Oxford walipata kiasi cha homoni ya cortisol kwenye mate ya mashabiki 40 kabla, wakati na baada ya mechi tatu za kombe la dunia.
Mashabiki wa Brazil
Kilichokuwa kikiwaweka watu kati hali ya wasiwasi mwingi ni hatua ya nusu fainali.
''Ilikuwa mechi ya kuogopesha- hivyo watu wengi walitoka wakilia,'' Daktari Newson ameiambia BBC.
Lakini mashabiki wamekuwa wakijipoza kwa kuzungumzia habari za ucheshi na kukumbatiana kupunguza msongo wa mawazo.
Daktari amependekeza viwanja vya mpira viwe vinawasha mwanga mdogo na kupiga muziki wa taratibu baada ya michezo.
''Vilabu vinaweza kutoa huduma ya vipimo vya moyo au vipimo vingine vya kiafya kwa mashabiki wao wakubwa ambao wako hatarini kupata matatizo ya moyo wakati wa mchezo.


EmoticonEmoticon