Mawakili Watoa Majibu Dhidi Ya Mashtaka Yanayomkabili Donald Trump

Donald Trump
Jopo la mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump kwa mara ya kwanza limetoa majibu rasmi kuhusiana na mashtaka dhidi yake likitaja kuwa "vita vikali" dhidi ya demokrasia.
Taarifa yao ilisema vifungu vya sheria kuhusu hoja ya kumuondoa rais havikutaja makosa yoyote yaliyofanywa na kuongeza kuwa ni ''njama'' ya jaribio la kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.
Kauli hiyo inakuja wakati Democrats wamewasilisha malalamishi yao kabla ya kuanza wa kesi hiyo wiki ijayo.
Bw. Trump ni rais wa tatu wa Marekani kukabili na mashtaka.
Anatuhumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka yake na kuzuia bunge la Congress kufanya uchunguzi. Amepinga kufanya kosa lolote na kutaja kesi dhidi yake kuwa "owongo".
Bunge hilo linaloongozwa na chama cha upinzani cha Democrats, lilipiga kura ya kutokuwa na imani na rais mwezi uliopita.
Bunge la Seneti,linaloongozwa na chama cha Republican cha Bw. Trump, litaamua ikiwa atashitakiwa na kumuondoa madarakani.


EmoticonEmoticon