Mbwana Samatta Kupata Nafasi Ya Kucheza Fainali

Mtanzania Mbwana Samatta usiku wa Jan 28 alikuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichocheza dhidi ya Leicester City katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Carabao Cup.
Mchezo wa kwanza uliochezwa King Power ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1, hivyo leo ndio ilikuwa hatma ya timu zote mbili.
Mchezo huo Samatta alicheza kwa dakika 66 na kutolewa na nafasi yake akaingia Keanan Devis, Aston Villa wakiingia fainali kwa ushindi wa 2-1  (agg 3-2) kwa magoli safi ya Targett dakika ya 12 na Trezeguet dakika za nyongeza.
Goli la Leicester lililofungwa na Iheanacho dakika ya 72 alikuwa na msaada tena, hivyo Aston Villa wakiwa na Samatta wanasubiri mshindi kati ya Man City na Man United ndio watacheza naeo fainali March 1 2020.
Photoscredit:Gettyimages


EmoticonEmoticon