Mfahamu Kijana Aliyevunja Rekodi Ya Ubakaji Kwa Wanaume Na Wanawake, Hukumu Yake

Reynhard Sinaga
Mwanaume mmoja ameshtakiwa kwa makosa 159 ya unyanyasaji kingono, yakiwemo makosa 136 ya ubakaji, jaji amesema kuwa labda mtu huyo hataachiwa huru tena kwa kuwa si mtu salama.

Reynhard Sinaga alikutwa na hatia ya kuwarubuni wanaume 48 nje ya kilabu cha Manchester na kuwapeleka katika makazi yake, ambapo aliwalewesha madawa na kuwafanyia vitendo viovu vya kingono -na kupiga picha matukio hayo.
Polisi wanasema kuwa, wana ushaidi unaomuhusisha Sinaga, mwenye umri wa miaka 36, ambaye alitajwa kwa mara ya kwanza kuhusika na udhalilishaji wa watu 190.
Mwendesha mashtaka wanasema kuwa Sinaga ni mbakaji aliyevunja rekodi katika historia ya Uingereza.
Mahakama imemuhukumu kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 30 gerezani.
Mwanafunzi huyo wa chuo kikuu tayari ameanza kutumikia miaka 20 gerezani , kwa kukutwa na hatia ya makosa mengine aliyoyafanya 2018 .
Ukiachilia mbali mshtaka mengine manne ambayo alikutwa nayo, kijana huyo mwenye uraia wa Indonesia alikutwa na hatia ya makosa 136 ya ubakaji, na majaribio 8 ya ubakaji, makosa 14 ya unyanyasaji wa kingono na kosa moja lingine linalohusisha sehemu za siri, dhidi ya waathirika 48.
Maafisa wa upelelezi wanasema kuwa wameshindwa kuwabaini waathirika 70 na sasa wanataka watu wote waliohisi kuwa walifanyiwa unyanyasaji na Sinaga kujitokeza.
Wakati wa shauri la kesi hiyo jaji Suzanne Goddard alisema kuwa Sinaga alihusika katika matukio kadhaa ya unyanyasaji wa kingono kwa vijana wadogo ambao walikuwa wanataka kufurahi na marafiki tu.
“Katika hukumu yangu, wewe ni mtu hatari sana ambaye unahitajika kuadhibiwa na kutoachiwa huru tena,” Jaji alimwambia mtuhumiwad – na kuongeza kuwa maamuzi hayo yamefanywa na bodi ya wafungwa.
Sinaga alikuwa anasubiri muda ambao watu wanaondoka kumbi za starehe kabla ya kuwarubuni kwenda kwenye nyumba yake iliyopo Montana mtaa wa Princess, mara nyingi alikuwa anawakaribisha kinywaji au kuwakodia gari.
Huwa anawalewesha kabla ya kuwafanyia vitendo vya ajabu huku wakiwa hawajitambui. Wengi wao wanapoamka huwa hawakumbuki kile ambacho kiliwatokea.
Wanafunzi ambao walikataa hukumu hiyo walidai kuwa waliridhia kupigwa picha huku wakijidai kuwa walikuwa wamesinzia ,jambo ambalo jaji alidai kuwa ni utetezi wa kipuuzi na uongo.
Katika shauri la kesi za awali, jaji alisema kuwa ana uhakika kuwa Sanaga alikuwa anatumia fomu inayoonyesha namna alivyowabaka watu.


EmoticonEmoticon