Miili Ya Marehemu Katika Ajali Ya Kobe Bryant Yatambuliwa, Picha Za Eneo La Tukio Zatolewa (PICHA)

Wataalam wa mataibabu na wa uchunguzi wa miili wameutambua mwili wa giwji wa zamani wa NBA Kobe Bryant  baada ya kupata miili ya watu wote tisa walioaga dunia katika ajali ya helikopta siku ya jumapili . 

Mwili wa Bryant ulitambuliwa pamoja na watu wengine watatu kutumia alama zao za vidole  siku mbili baada ya mkasa huo kutokea.

Wakati huo huo maafisa  wa uchunguzi wa ajali wameshatembelea eneo la mkasa  kwa ukaguzi  na kulikabidhi kwa maamlaka za eneo hilo.
Awali wachunguzi walionekana wakitumia ndege ndogo za droni kuiga picha eneo hilo na wakiafanya ukaguzi  katika mabaki ya helikopta hiyo  yaliyotapakaa  sehemu ya upana  wa mita 180.

Mwili wa rubani Ara Zobayan na kocha wa  baseball  John Altobelli na Sarah Chester pia imetambuliwa .
Bryant mwenye umri wa miaka 41  alikuwa akisafiri  pamoja na binti yake Gianna na watu wengine saba  wakati helikopta hiyo Sikorsky S-76  ilipogonga mlima na kuanguka  Calabasas,  kaskazini magharibi mwa LA .


EmoticonEmoticon