Mo Dewji Ajiuzulu Rasmi Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) ametangaza kuachia ngazi kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya Mtibwa na Simba 1-0 kwenye mechi iliyopigwa usiku wa Jan13.

Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mo alisema: “Baada ya kulipa mishahara inayofikia Sh4 bilioni kwa mwaka, najiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Nitabaki kuwa mwekezaji na nitazingatia kukuza miundombinu ya soka la vijana.”

Mtibwa ambao walionekana kucheza soka safi na kumiliki mchezo huo, ilipata bao lake la ushindi dakika ya 38 kupitia kwa Awadh Salum, ambaye alipenya katikati ya msitu wa walinzi wa Simba.

Uamuzi wa Mo kuachia wadhifa huo Simba, umeibua sintofahamu sio kwa wanachama tu, bali kuhusu pia hatima ya bodi hiyo.


EmoticonEmoticon