Mwanafunzi Ajiua Kisa Kurudia Darasa

Mwanafunzi  mmoja katika shule ya  ya msingi ya Amani huko Jomvu ,Mombasa amejiua baada ya kutakiwa kurudia darasa la sita . 

Rehena Kura hakutaka kurudia  darasa lakini shule hiyo ilisisitiza kwamba lazima angerejelea darasa ambalo alisoma mwaka wote jana . Rehema  ambaye hajakuwa akiripoti shuleni kila siku tangu shule zifunguliwe mapema wiki hii amejitia kitanzi katika nyumba ya wazazi wake .

Mwili wake  ulipatikana na dadake  ukining’inia darini  katika nyumba yao . Mamake , Sada Nganda amesema alizungumza na bintite jumatano asubuhi  ambapo alimwambia kwamba hakuwa akihisi vyema kasha akamshauri apumzike .

Dadake amesema Rehema hakutaka kurudia darasa la sita na uamuzi wa kumlazimisha kufanya hivyo ulimtia hamaki sana. 

Naibu kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Jomvu Jason Odhiambo amesema polisi wanachunguza ripoti kwamba maafisa wa shule hiyo wanawalazimisha wanafunzi kurejelea madarasa .
Credits:Radiojambo


EmoticonEmoticon