Mwisho Wa Matumizi Ya Windows 7 Jan 2020, Imependekezwa Kutumia Windows 10

Windows 7 To 10
Kama unatumia Windows 7 kwenye kompyuta yako basi muda wa kusasisha (upgrade) kwenda Windows 10 umefika. Microsoft wameiweka tarehe 14 Januari 2020 kama mwisho rasmi wa utumiaji wa Windows 7.
Kuanzia tarehe 14 January kompyuta inayotumia Windows 7 isitegemee kupata updates (masasisho) ya aina yeyote ya kuhakikisha usalama wa data kwenye kompyuta zao.Windows 10
Microsoft, wanalenga watumiaji wote wahamie katika programu endeshaji yao ya kisasa ya Windows 10.
Kutumia toleo la Windows ambalo halipati masasisho (updates) ya kiusalama ni hatari kwa usalama wa data zako. 

Kompyuta zinazotumia Windows 7 zinakuwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na virusi au programu za udukuzi wa data (ransomware).
Statistics
Data kutoka shirika la data la NetMarketShare linaonesha utumiaji wa Windows 10 kukua, kufikia Disemba mwaka 2019 asilimia 54.62 ya kompyuta zinazotumia intaneti zilikuwa zinatumia Windows 10, huku Windos 7 ikichukua asilimia 26.64 tuu. Asilimia zingine zikichukuliwa na Mac OS, Linux na matoleo mengine ya programu endeshaji.


EmoticonEmoticon