Ole Gunnar Solskjaer Atoa Ya Moyoni Kuhusiana Na Manchester City

Ole Gunnar Solskjaer
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema amependa namna Pep Guardiola alivyoisuka Manchester City.
Pep Guardiola
Kauli ya Solskjaer imekuja ukiwa umebaki muda mfupi kabla ya timu hizo kuvaana katika mchezo wa Derby ya Manchester kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Timu hizo zitacheza mchezo wa Kombe la Ligi huku Man United ikiwa kumbukumbu ya kuilaza Man City mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo unarudisha nyuma miaka mitatu ambapo Man United iliilaza Man City bao 1-0 lililofungwa na Juan Mata Oktoba 26, 2016 katika raundi ya nne kwenye uwanja huo.
wachezaji wa Man City
Solskjaer (46) alisema wachezaji wa Man City wanacheza kwa kiwango bora na siku zote wamekuwa na mchezo mzuri.

Man City inaivaa Man United ikiwa mbele kwa pointi 13 katika Ligi Kuu England huku mahasimu wao wakishindwa kuonyesha kiwango bora tangu kuanza mwaka huu.

Man United ilcharazwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal kabla ya kucheza katika kiwango cha chini ilipotoka suluhu na Wolves ambapo haikupiga shuti langoni mwa wapinzani wao.

“Imekuja kivingine katika muda mwingine. Walipokuja wamiliki wapya, timu inacheza kwa kiwango bora. Inaendelea kuimarika na miongoni mwa klabu kubwa duniani,”alisema kocha huyo.


EmoticonEmoticon