Raisi Atoa Tahadhari Baada Ya Virusi Vipya Vinavyoua Kusambaa Kwa Kasi

Mlipuko wa virusi vipya vinavyouwa vinasambaa kwa kasi, Rais Xi Jinping ametoa tahadhari baada ya kufanya kikao maalum katika siku ya mwaka mpya wa Lunar.
Rais aliwaambia maofisa wa ngazi za juu kuwa nchi iko kwenye hali ya hatari kubwa , kwa mujibu wa televisheni ya taifa.
Virusi vya corona tayari vimeuwa watu wapatao 41 na wengine 1,400 wameambukizwa tangu virusi hivyo vigundulike huko Wuhan.
Tayari miji mingi imeweka katazo la kusafiri kwa watu wake.
Na siku ya jumapili hata magari binafsi hayataruhusiwa kutoka Wuhan, eneo ambalo virusi hivyo viibainika kwa kwa mara ya kwanza.
Hospitali nyingine ya dharura inajengwa na inategemewa kuwa ndani ya wiki , itaweza kuwahudumia wagonjwa wapya 1,300, na itamalizika kujengwa ndani ya nusu mwezi, gazeti la serikali la la People's Daily limeripoti.
Huu ni mradi wa pili wa ujenzi wa hospitali ambao unafanyika, hospitali nyingine ujenzi wake umeanza tayari na inategemea kuchukua wagonjwa 1000.
Kikosi maalum cha wanajeshi ambao ni madaktari tayari wameenda jimbo la Hubei , eneo ambalo Wuhan ipo.
Angalizo la virus hivi lilitolewa kwa China na maeneo mengine duniani tangu mwezi Desemba, wakati virusi hivyo vilipogundulika..
Sherehe za mwaka mpya wa China ambao mwaka huu ni wa panya zilianza siku ya jumamosi, lakini tafrija za sherehe hizo zilisitishwa kufanyika katika maeneo mengi ya nchi hiyo.
Mpakani wasafiri wamekuwa wakipimwa joto lao kuangaliwa kama wana hali yoyote ya homa na usafiri wa tren umefungwa pia katika miji kadhaa.
Huko Hong Kong, taarifa ya dharura imeongeza muda wa likizo wa shule .
Nchi kadhaa nyingine zimeanza kutibia wagonjwa wake kwa uangalizi wa peke yake.


EmoticonEmoticon