Sababu Za Instagram Kuhamisha Kitufe Cha IGTV, Msemaji Afunguka

Kama wewe ni mtumiaji wa sehemu ya IGTV kupitia app ya instagram basi inawezekana tayari umeona kwa sasa ni vigumu kuweka au kupost video mpya ya IGTV kupitia app ya Instagram, hii ni kwa sababu Instagram imeondoa kitufe cha IGTV kupitia app ya Instagram.

“Tunapoendelea kufanya kazi ili kuifanya iwe rahisi kwa watu kuunda na kugundua yaliyomo kwenye IGTV, tumejifunza kuwa watu wengi wanapata yaliyomo kwenye IGTV kupitia preview Feed, channel ya IGTV, kupitia app ya IGTV, pamoja na kupitia profile mbalimbali. 


Ni wachache sana wanaobofya kwenye ikoni ya IGTV kwenye kona ya juu ya kulia ya skrini ya nyumbani kwenye programu ya Instagram ” msemaji wa kampuni ya Facebook alikiambia chanzo kimoja.

“Sisi kila wakati tunakusudia kufanya app za Instagram kuwa rahisi kutumia iwezekanavyo, kwa hivyo kwa sasa tunaondoa ikoni (Icon ya IGTV) hii kulingana na maoni kutoka kwa watumiaji wetu.”

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji huyo, watumiaji wa instagram watakuwa hawaitaji app ya IGTV kama wanataka kuangalia video mbalimbali za IGTV kwani zitakuwa zinaonekana kwenye profile za watumiaji, kupitia Tab ya Explore, pamoja na kupitia kwenye home feed.
Kwa wale ambao wanataka kuweka video za IGTV sasa inabidi kupitia sehemu ya Explore ambapo utaona kitufe cha IGTV upande wa kushoto juu, ambapo baada ya kubofya hapo utaweza kuona video za IGTV pamoja na sehemu ya kuweka video ambayo ipo juu upande wa kulia kwenye ukurasa huo wa IGTV.


EmoticonEmoticon