Sababu Zilizomfanya Kylie Jenner Kutoa Billion 2 Ni Hizi

Kylie Jenner
Macho na masikio ya dunia yote yapo nchini Australia ambapo moto mkubwa unateketeza misitu na kusababisha vifo vya wanyama na maliasili, Mwanadada Kylie Jenner mwenye utajiri wa dola Bilioni za Kimarekani ameguswa na hilo na kuamua kutoa mchango wake kusaidia.

Kylie amechangia kiasi cha dola milioni 1 ambazo ni sawa na Bilioni 2 za Kitanzania kwenda kwenye mifuko ya taasisi 5 kusaidia kuokoa wanyama na makazi pamoja na watu wote walioathirika na moto huo.

Hivi karibuni familia ya Kardashian ilikumbwa na kashfa ya kutosaidia watu wenye matatizo licha ya kuwa na utajiri mwingi. Kim Kardashian aliweka wazi kuwa sio lazima kila wanachofanya basi ni lazima kiwekwe wazi.


EmoticonEmoticon