Tazama Trailer Ya Filamu Ya Fast And Furious 9 Na Fahamu Tarehe Kamili Ya Filamu Hiyo Kutoka (VIDEO)

Fast & Furious 9
Fast & Furious 9 baada ya kuchiwa kipande kidogo last week, siku ya Jan 31 Universal Picture wameachia official trailer ya filamu hiyo ambayo inategemewa kuingia katika cinema rasmi May 22 mwaka huu huku ikiwa imesheheni mastaa kibao.
Vin Diesel & John Cena Fast 9
Vichwa wa filamu hiyo inayotegemewa kwa hamu kutazamwa na watu ni Vin Diesel, Charlize Theron, John Cena. Imeongozwa na Justin Lin.

Sio hii filamu tu huwa inategemewa kwa mauzo bali hata soundtrack zake huwa zinafanyaga vizuri sana katika mauzo hasa ya album, ambapo mwaka huu hedlines za ngoma zimewakutanisha wakali kama Cardi B, Wiz Khalifa, Charlie Puth, Ozuna, Ludacris na wengine kibao.

Filamu hizi za Fast & Furious zilianza msimu wake wa kwanza kutolewa tangu mwaka 2001, zinatajwa kuwa filamu zinazoingiza pesa nyingi zaidi kutokana na mauzo yake katika soko la filamu duniani.

TAZAMA TRAILER HAPA


EmoticonEmoticon