Ugunduzi Wa Mfumo Mpya Wa Kinga Wa Saratani Zote Wagunduliwa

Ugunduzi wa mfumo mpya wa kinga unaweza kutumika kutibu aina zote za saratani, wanasema wanasayansi.

Kundi hilo kutoka chuo kikuu cha Cardiff liligundua mtindo wa kutibu saratani ya tezi dume, ile ya matiti ya mapafu na aina nyengine za saratani katika vipimo vya maabara.

Matokeo yake yaliochapishwa katika jaradi la kinga asli ,hayajajaribiwa miongoni mwa wagonjwa lakini wanasayansi hao wanasema yana uwezo mkubwa.

Wataalam wanasema kwamba ijapokuwa kazi hiyo ilikuwa hatua za kwanza ilikuwa inafurahisha.

Mfumo wetu wa kinga ni jinsi mwili wetu unavyoweza kujilinda dhidi ya maambukizi lakini pia unashambulia seli zilizo na saratani.

Wanasayansi hao walikuwa wakitafuta njia ambazo hazijagunduliwa kuhusu jinsi mfumo wetu wa kinga unavyoshambulia uvimbe unaosababisha saratani.
Kile walichogundua ni seli aina T ndani ya damu. Hii ni seli katika kinga ambayo inaweza kupima iwapo kuna tishio mwilini ambalo linafaa kuondolewa.

Tofauti yake ni kwamba seli hiyo inaweza kushambulia aina tofauti za saratani.

Kuna fursa hapa ya kutibu kila mgonjwa, mtafiti profesa Andrew Sewell aliambia BBC.

Aliongozea: Awali hakuna aliyeamini kwamba hili linaweza kufanyika. Inatoa fursa ya tiba moja kutibu saratani zote, seli moja aina ya T inayoweza kuharibu aina tofauti ya saratani miongoni mwa waathiriwa.

Seli aina ya T zina uwezo wa kubaini kiwango cha kemikali mwilini.

Kundi hilo la Cardif liligundua seli aina ya T na receptor yake ambayo inaweza kugundua na kuuwa idadi kubwa ya seli za saratani katika maabara ikiwemo katika mapafu, ngozi, damu, koloni, matiti, tezi dume, mayai na shingo ya uzazi.

Kitu muhimu ni kwamba iliwacha tishu muhimu bila kuathiriwa.


EmoticonEmoticon