Ukweli Wa Taarifa Za Kifo Cha Mchezaji Kobe Bryant Na Mwanaye

Kobe Bryant Na Mwanaye Gianna Maria Onore
Mchezaji wa zamani wa Los Angeles Lakers Kobe Bryant amefariki dunia kwa ajali ya ndege ambapo Afisa wa polisi Alex Villanueva alisema kuwa helkopta inaonyesha uwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.
Kobe Bryant Na Mwanaye Gianna Maria Onore
Taarifa zinasema kwamba Binti wa marehemu Kobe Bryant, Gianna Maria Onore (13) ni miongoni mwa waliofariki dunia kwenye ajali ya helikopta ambayo imeua watu watano.
NBA ilitoa tamko linalosema kuwa ,imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna" mwenye umri wa miaka 13.
"Kwa misimu 20 , Kobe alituonyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi," 
Kobe Bryant Na King Lebron James
Hii ndio ilikuwa tweet ya mwisho ya Kobe Bryant ambapo jana alimpongeza LeBron James ambaye ameipiku rekodi yake ya ufungaji (33,643) kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote kwenye NBA. King James akifikisha Pointi (33,644) na kukaa kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Karl Malone na Kareem Abdul - Jabbar.


EmoticonEmoticon