Usafiri Wa Umma Wasitishwa Kutokana Na Mlipuko Wa Virusi Vya Ugonjwa Wa Corona

China
China imefanya maamuzi magumu ya kusitisha usafiri wa umma hasa katika mkoa wa Wuhan,unaokaliwa na watu karibu milioni tisa, wakati wa mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona.
Watu wanaoishi katika jiji hilo wameambiwa wasiondoke nje ya mji huo , na uwanja wa ndege na vituo vya treni vitafungwa kwa abiria wanaotoka nje ya eneo hilo.
Basi, reli za chini ya ardhi, feri, na mitandao ya uchukuzi wa umbali mrefu itasitishwa kuanzia leo Alhamisi.
Virusi vipya vimeenea kutoka Wuhan hadi majimbo kadhaa ya China, Marekani, Thailand na Korea Kusini.
China
Virusi, vinavyojulikana kama 2019-nCoV, inaarifiwa kuwa ni aina mpya ambavyo havijatambuliwa awali kuwa vinaathari kwa wanaadamu.
Taarifa hii yenye kuogofya ulimwenguni kutokana na kasi ya ueneaji wa ugonjwa huo, mlipuko huo umewauwa watu 17, na kuna kesi 440 zilizothibitishwa.
Wachunguzi wa afya wanaarifu kuwa Virusi hiyo ilitoka katika soko la vyakula vya baharini ambalo "lilichanganya vyakula hivyo na shughuli haramu za wanyama wa porini".
Kama hiyo haitoshi Viongozi huko Hong Kong pia waliripoti kesi mbili za kwanza za eneo hilo.
Kama utakumbuka vizuri kulikuwa na virusi vya Sars ambavyo viliwauwa karibu watu 800 ulimwenguni mwanzoni mwa miaka ya 2000 na madaktari wanaarifu kuwa navyo ni jamii ya virusi vya Corona.
Mkutano wa kutathmini hatari za kiafya zinazokabili ulimwenguni ulisitishwa ili kuamua ikiwa inapaswa kutangazwa dharura ya afya kimataifa kama ilivyotokea wakati wa homa ya nguruwe na ugonjwa wa Ebola pia.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon