Virusi Vipya Vya Ugonjwa Vinavyosambaa Kwa Kasi Nchini China Na Maeneo Ya Jirani

Virusi vipya huenda vikazaana na kusambaa katika maeneo ya mbali, maafisa wa afya wa China wameonya, huku wakiongeza juhudi za kudhibiti maambukizi.
Idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo imeongezeka na kufikia tisa huku visa vingine 440 vikithibitishwa, walisema.
Afisa wa tume ya kitaifa ya afya amekiri kuwa nchi hiyo kwa sasa iko "katika awamu muhimu" ya kuzuia na kudhibiti kusambaa kwake.
Siku ya Jumanne , mamlaka ilithibitisha usambazaji wa virusi hivyo kupitia binadamu.
Katika taarifa ya kwanza kwa umma tangu mwanzo wa mlipuko wa ugonjwa huo, naibu waziri wa tume ya afya ya China, Li Bin alisema kuna ushahidi kuwa ugonjwa huo "unasambazwa kupitia mirija ya kutoa pumzi".
Lakini China haijafanikiwa kubaini chanzo halisi cha virusi hivyo.
"Japo mfumo wa maambukizi haujaeleweka, kuna uwezekano virusi hivi vinaweza kuzaana na hatari ya kusambaa," alisema Bw. Li.
Onyo hilo linakuja wakati mamilioni ya watu kote nchini China wakisafiri kutoka eneo moja hadi lingine kuadhimisha mwaka mpya wa Lunar.
Maelfu ya wengine wanasafiri nje ya nchi.


EmoticonEmoticon