Yaliyomkuta Mchungaji Baada Ya Kumuua Mke Wake Kanisani


Mchungaji wa kanisa moja mjini Mombasa pwani ya Kenya amezua gumzo baada ya tukio la kujikata koo baada ya kumdunga kisu mke wake mara kadhaa wakati wa ibada ya Jumapili.
Bwana Elisha Misiko, 55, alikuwa mhubiri wa kanisa hilo katika mtaa wa Bamburi akishirikiana na mkewe Ann Mghoi
Jamaa, marafiki na waumini wa kanisa hilo wameliambia gazeti la Nation kuwa kisa hicho kilitokana na mzozo wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa kanisa hilo.
"Watu hawa wamekuwa wakiendesha kanisa hili kwa zaidi ya miaka minane lakini walitofautiana miezi michache iliyopita."Mzee wa mtaa wa cha Chembani Mtengo Amuri alisema.
Mchungaji huyo alimlaumu mkewe, Ann Mghoi kwa kupanga njama ya kumfukuza kutoka kanisa hilo ambalo anadai kulianzisha.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, waumini walidai kuwa Bw.Misiko aliingia kanisani mwendo wa saa tatu asubuhi na kukaa safu ya mbele karibu na mke wake.
Wakati ibada ikiendelea, wanasemsa aliamka ghafla kwenye kiti chake na kumshambulia mke wake kwa visu viwili ambavyo alikuwa ameficha ndani ya koti lake.
Bw. Misiko alimdunga kisu mara kadhaa Bi Mghoi kabla ya waumini waliokumbwa na mshangao kuingilia kati kumuokoa na kumkimbiza katika hospitali kuu pwani, ambako alifariki akipata matibabu.
Ni wakati wa purukushani ya kumuokoa Bi Mghoi ilipokuwa ikiendelea ambapo Bw. misiko alijitoa uhai.
Rafiki wa karibu wa familia hiyo Bi Janet Tole, alisema kuwa wanandoa hao walizozana kwa muda mrefu na kutengana kwa miezi michache iliyopita.
Alisema kuwa Bw. Misiko, aliwahi kumtishia maisha Bi Mghoi mara kadhaa, madai ambayo yalithibitishwa na kijiratasi ambacho kiliandikwa na mchungaji huyokabla ya kutekeleza mauaji hayo.
"Alisema kuwa mkee alimzuia kuona watoto wao walipotengana," aliongeza Bi Tole, mmoja wa watu waliomkimbiza hospitali Bi Mghoi baada ya kudungwa kisu.
Muumini mwingine alidai aliliambia gazeti la Nation kuwa Bwana Misiko na Bi Mghoi walipigana ndani ya nyumba yao kabla ya kuanza kwa ibada.
Kamanda wa polisi wilaya Julius Kiragu amethibitisha kutokea kwa kisa hicho na kuongeza kuwa mwanamke huyo alidungwa kisu mgongoni, mikononi na tumboni .
Bw. Kiragu alisema kuwa , Misiko alipanga tukio hiloo kwa muda mrefu, kama ilivyobainika katika kijikaratasi alichoandika kabla ya kujiua ambapo alimlaumu mkewe kwa kumdhalilisha.
"Watu kadhaa wameandikisha taarifa kuthibitisha kuwa tukio hili limetokana hatua ya mke kujaribu kumfukuza mumewe katika kanisa alilopambana kulijenga," aliongeza.
Kamanda huyo wa polisi aliripoti kuwa mchungaji huyo alifariki ndani ya kanisa hilo na kwamba mwili wake umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali kuu ya mkoa wa Pwani.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon