50 Cent Ajibu Swali, Kati Ya Filamu Na Muziki Wapi Panamuingizia Mkwanja Mrefu?

Rapa 50 Cent Kwenye headsline nyingine wiki hii baada ya kuweka wazi kuwa filamu ina mtonyo mwingi zaidi kuliko muziki.

Kupitia mahojiano yake na kipindi cha Cigar Talk, 50 amefunguka alipoulizwa kipi kina mtonyo mrefu zaidi kati ya Muziki na Filamu na kukiri wazi kuwa Filamu ina pesa zaidi kuliko muziki.

Aidha 50 amebainisha kuwa, wakati anafanya muziki chanzo chake kikubwa cha mtonyo kilikua ni Matamasha, tofauti na Filamu ambapo anaingiza mtonyo mwingi zaidi kutoka kwenye Televisheni.


EmoticonEmoticon