Familia Ya Marehemu Rais msataafu Daniel Moi Yafunguka Kuhusiana Na Maziko Yake

Rais msataafu Daniel Moi atazikwa nyumbani kwake  Kabaraka huko Baringo  familia yake imesema . Ikiongozwa na raymond Moi familia hiyo hata hivyo imesema tarehe ya maazishi ya mwendazake Moi itatangazwa baadaye.

Raymond amesema maazishi ya Moi sasa yatashughulikiwa na jeshi  na kuanzia sasa mawasiliano yatatolewa na  msemaji wa serikali au afisa mwingine yeyote wa ngazi ya juu serikalini.

Tunataka kulishukuru jeshi na maafisa wa serikali kwa  kuchukua hatua za haraka kuingilia kati katika utaratibu mzima wa kumpa heshima za mwisho na  ombi letu kwamba Mola atatupa nguvu za kustahimili kumpoteza Mzee". amesema Raymond ambaye ni mwanawe Mzee Moi na pia mbunge wa Rongai.

Awali Naibu wa rais William Ruto  alisema mkuu wa utumishi wa umma  Joseph Kinyua  atachukua usimamizi wa mipango ya maazishi .Ruto alikuwa akiwahutubia wanahabari katika afisi yake ya  Jumba la Harambee
Photocredit:thestar
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon