Habari 5 Kubwa Za Michezo Alhamisi Feb 6

Messi Man City
1. Manchester City wanaamini watakuwa chaguo la kwanza la nyota wa Argentina Lionel Messi endapo ataamua kuihama Barcelona baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu. 
2. Mipango ya Liverpool na Manchester United ya kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, itategemeana na mustakabali wa kiungo Philippe Coutinho, 27, wa Bayern Munich.
3. Manchester City wapo katika wakati mgumu wa kumzuia winga wao Leroy Sane, 24, asihamie klabu ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu baada ya mchezaji huyo kubadili wakala wake.
4. Chelsea na Manchester United wanajiandaa kupambana vikali kuwania kumsajili mshambuliaji wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. 
5. Mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona Eric Abidal amegusia kuwa klabu hiyo huenda ikajaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mwishoni mwa msimu.


EmoticonEmoticon