Habari 5 Kubwa Za Michezo Ijumaa Feb 7

1.Manchester United wamepunguza dau la kumuuza kiungo wao nyota Paul Pogba, 26, kwa pauni milioni 30. Sasa United watakubali kumuuza Mfaransa huyo kwa pauni milioni 150. Pogba ameondolewa kwenye msafara wa Manchester United nchini Uhispania.
Hata hivyo Klabu hiyo imejiondoa katika mbio za kumsajili Martinez kutokana na mkataba wake kuweka kiwango cha mauzo cha pauni milioni 94 na pia wanataka "si chini ya" pauni milioni 15 ili wakubali kumuuza beki wao Chris Smalling, 30, ambaye yupo Roma kwa mkopo.
2. Barcelona wanajipanga kumsajili winga wa Wolves Adama Traore, 24, mwishoni mwa msimu huu. Pia kuna taarifa zinasoma kwamba hawatamlipa chochote wakala Jorge Mendes baada ya kumsajili mshambuliaji Francisco Trincao, 20, kutoka Braga.
3.Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anapanga kukisuka upya kikosi cha kwanza cha Gunners ambapo anatarajiwa kuwauza mshambuliaji wa Gabon striker Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 28 na kiungo Mjerumani Mesut Ozil, 31.
4. Chelsea imeibuka kuwa chaguo namba moja la kipa wa Cameroon na Ajax Andre Onana, 23, kuhamia mwishoni mwa msimu. Hayo yanajiri wakati Chelsea inatathmini iwapo wamuuze kipa wao Kepa Arrizabalaga, 25. 
5. Beki wa Tottenham Muingereza Japhet Tanganga, 20, yupo katika mazungumzo na klabu ili kuongezewa mshahara kwa asilimia 1,500 Kurosawa malipo ya sasa ya pauni 1,000 kwa wiki. Maboresho hayo yanakuja baada ya Tanganga kuingia kwenye kikosi cha kwanza.
Pia kuna taarifa zinazosema kwamba mke wa mshambuliaji mpya wa Hertha Berlin Krzysztof Piatek, 24, amekanusha ripoti kuwa alimzuia mumewe kuhamia Tottenham.


EmoticonEmoticon