Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumamosi Feb 8

1.Chelsea inasemekana kwamba iko mbioni wasajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, na mshambuliji wa Lyon Moussa Dembele, 23. Pia  timu hiyo kufikia makubaliano na kiungo wa kati wa Uingereza Tino Anjorin, 18, na mlinzi wa raia wa Uholanzi Ian Maatsen, 17.

2. Juventus inamwinda mshambuliaji wa Chelsea na Italia Emerson Palmieri, 25, kama mmoja wa wale wanaomlenga wakati wa usajili msimu wa joto.

3. Barcelona imeonyesha nia ya kumsajili tena raia wa Uhispania Adama Traore baada ya kuhofia kwamba huenda Real Madrid ikakimbilia kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 24. 

4. Liverpool haitarajiwi kusaini mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uingereza Adam Lallana, 31, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

5. Tottenham, Burnley na Aston Villa zote zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliajo wa Fenerbahce raia wa Uturuki Vedat Muriqi, 25.


EmoticonEmoticon