Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumanne Feb 11

Philippe Coutinho
1.Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona kwa kitita cha chini ya £77m mwisho wa msimu huu huku Manchester United, Chelsea, Manchester City, Tottenham na Liverpool zote zikimnyatia.

2. Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Unai Emery amesema kwamba klabu hiyo imekuwa ikishuka wakati alipowasili na kuwashutumu baadhi ya wachezaji kwa kutokuwa na tabia nzuri.

3. Chelsea, Aston Villa na Newcastle United zote zinataka kumsaini beki wa kushoto wa Wigan Antonee Robinson baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kukosa kuhamia katika klabu ya AC Milan katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.

4. Mipango ya 2020-21 ya klabu ya Manchester imesitishwa kutokana na virusi vya corona baada ya klabu hiyo kupanga kwenda China.

5. Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amekataa kukubali kwamba timu yake haitakuwa miongoni mwa timu nne bora katika ligi ya Uingereza licha ya kuwa polinti 10 nyumba ya timu iliopo katika nafasi ya nne Chelsea.


EmoticonEmoticon