Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumanne Feb 4

Frank Lampard, Keppa & Nick Pope
1.Kocha wa Chelsea Frank Lampard yuko kwenye mpambano na klabu hiyo kuhusu kumuuza mlinda mlango wa uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, Huku akimtaka mlinda mlango wa Burnley na England Nick Pope, 27 kuchukua nafasi hiyo
2. Real Madrid wako tayari kumsajili Kylian Mbappe, 21.
3. Liverpool, Manchester United na Chelsea wanamtolea macho Timo Werner, 23, Werner amesema atakuwa tayari kuhamia klabu itakayofaa. Mshambuliaji huyo wa Ujerumani amefunga magoli 25 katika michuano yote ya RB Leipzig msimu huu.
4. Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 30, huenda akahamia Super League ya China au Ligi kuu ya Marekani, kuliko ligi kuu ya Uingereza, atakapoiacha klabu yake ya Uhispania. 
5. Liverpool wana shauku ya kufunga mkataba wa muda mrefu na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Virgil van Dijk, 28, na mlinda mlango Alisson.


EmoticonEmoticon