Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumapili Feb 2

1.Klabu ya Juventus inapanga kutenga paundi za Uingereza milioni 150 wakati wa kipindi cha majira ya joto kumnasa beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 28.

2. Klabu ya FC Barcelona inaelekea kufikia makubaliano ya kumnasa winga wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Chelsea, William mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu.

3. Juventus tayari imeanza maandalizi ya majira ya joto kupata saini ya kiungo wa kimataifa Sandro Tonali mwenye umri wa miaka 19 kutoka klabu ya Brescia pamoja na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Manchester United Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26.

4. Meneja wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amezuia uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 31 kwenda kujiunga na klabu moja ya nchini Qatar mwezi Januari.

5. Meneja wa klabu ya Everton, Carlo Ancelotti ameionya klabu ya FC Barcelona kuwa inapoteza muda wake kwa kujaribu kuwasilisha ofa ya juu zaidi kumnasa mshambuliaji wake wa Kibrazil Richarlison mwenye umri wa miaka 22, wakati wa kipindi cha majira ya joto. 


EmoticonEmoticon