Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumapili Feb 9

Leo Messi Barcelona
1.Manchester City wako tayari kukubali kushindwa katika harakati zao za kumpata Lionel Messi katika msimu ujao wa ligi ya Premier baada ya kuarifiwa kwamba mshambuliaji huyo wa Argentina, 32, hana mpango wa kuondoka Barcelona.
2. Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Brazil midfielder Philippe Coutinho, 27 ambaye kwasasa yuko Bayern Munich kwa mkopo, ataruhusiwa kuondoka kwa £77m ikiwa ni kiasi kidogo cha pesa huku Manchester United na iliyokuwa klabu yake Liverpool zikisemekana kuwa na nia ya kumsajili.
3. Mchezaji wa Manchester City Raheem Sterling anaamini kwamba atakuwa sawa katika Champions League kwenye mechi dhidi ya Real Madrid, ambao wanataka kumsajili mshambuliaji huyo, 25.
4. Grealish angependelea kujiunga na Manchester United katika msimu wa usajili ujao iwapo ataondoka Aston Villa licha ya tetesi kwamba Barcelona na Real Madrid wameashiria kuwa na nia ya kumsajili. 
5. Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 29, anasemekana kwamba huenda akaondoka Juventus, akiwa amesaini mkataba wa miaka minne pekee na Italia mwaka jana. 


EmoticonEmoticon