Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatano Feb 5

Leroy Sane
1.Juventus wanatathmini juu ya kumsajili winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, ambaye pia anawindwa na Bayern Munich.

2. Klabu ya Chelsea inajipanga kumpa kocha Frank Lampard kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 23.

3. Kocha wa Man City Pep Guardiola anataka kusajili walinzi wa kati wawili hatua ambayo inazidi kuweka wingu jeusi kwa mustakabali wa beki wa England John Stones, 25.

4. Wakala wa winga Gareth Bale, 30, amekanusha kuwa Tottenham ilituma ofa ya usajili kwa klabu ya Real Madrid kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

5. Manchester United wanajiandaa kutoa dau nono ili kumsajili kiungo wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, mwishoni mwa msimu. Pia wanamtaka Grealish kutokana na uwezekano mkubwa kwa chaguo lao la awali James Maddison, 23, kukaribia kusaini mkataba mpya na Leicester City.

Tukisalia hapo Man U, wanatarajia kipa wao raia wa Argentina Sergio Romero, 32, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu sambamba na kipa wao namba tatu Lee Grant, 37. 


EmoticonEmoticon