Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatatu Feb 3

Cavani & Bekham
1.Timu inayomilikiwa na mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United David Beckham, Inter Miami iliyopo Marekani inataka kuoneza nguvu ya kumsajili Cavani pale mkataba wake na PSG utakapofika tamati mwishoni mwa msimu.

2.Winga raia wa Brazil Willian, 31, angependelea kusaini mkataba mpya utakaombakiza Chelsea kuliko kujiunga na mabingwa wa Uhispania Barcelona. Pia Barcelona wametupilia mbali ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli Fernando Llorente, 34.

3.Raisi wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amedai kuwa klabu hiyo "isingekubali kutapeliwa" baada ya kushindikana usajili wa streka wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani.

4.Liverpool wanajipanga kumsajili mshambuliaji kinda na machachari wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu.

5.Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka kusajili kipa mpya baada ya kuporomoka kiwango cha kipa Kepa Arrizabalaga, 25.


EmoticonEmoticon