Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatatu Feb 10

Roberto Firmino & Philippe Coutinho
1.Bayern Munich wanapanga kutoa dau la pauni milioni 75m ili kumnasa msahambuliaji wa wa Liverpool na Brazil Roberto Firmino, 28, na pia wanataka winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, kuungana nae.

2. Klopp pia anapiga hesabu za kumrejesha Anfield kiungo wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Bayern Munich. Pia Klopp anamfanya kiungo wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, kama kipaumbele chake cha kwanza kwenye usajili wa mwisho wa msimu.

3. Kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, anatarajiwa kuomba kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu, akibakiza miezi 12 katika mkataba wake.

4. Kipengele cha mauzo kwenye mkataba wa beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, kitakuwa wazi kuanzia mwezi Juni kwa thamani ya pauni 127. Beki huyo amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Man United.

5. Kiungo wa Chelsea Italia Jorginho, 28, atakuwa mwenye furaha kuungana tena na kocha Maurizio Sarri Juventus, ameeleza wakala wake.


EmoticonEmoticon