Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi Feb 13

Tetesi za soka Ulaya
1.Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo, 30, amepigwa marufuku katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo kutokana na hofu ya hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

2. Mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, amekataa uwezekano wa kurudi katika klabu ya Liverpool akidai kwamba yuko katika safari.

3. Liverpool itakabiliana na Real Madrid katika kuwania saini ya kiungo a kati wa Inter Milan Marcelo Brozovic, 27, mwisho wa msimu huu .

4. Mkufunzi wa Juventus Maurizio Sarri amekiri kwamba Aaron Ramsey, 29, hajapata mambo kuwa rahisi wakati wa kipindi chake cha jeraha nchini Itali , na kuzua uvumi kwamba anapanga kurudi katika ligi ya England huku Arsenal, Manchester United, Liverpool na Chelsea zikihusishwa na uhamisho wake.

5. Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti, 60, tayari ana matumaini kwamba kandarasi yake itaongezwa katika uwanja wa Goodison Park baada ya kutia saini kandarasi mnamo mwezi Disemba. 


EmoticonEmoticon