Habari 5 Kubwa Za Soka Alhamisi Feb 20


1.Klabu ya Manchester United inaimani kuwa itamnasa mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu, lakini kwanza itawapasa kufuzu kwa mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya.

2. Klabu ya Juventus imewaorodhesha mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus (22) pamoja na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi (27) kama kipaumbele katika dirisha l usajili la mwishoni mwa msimu.

3. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kuwa hakumpanga kiungo Matteo Guendouzi, 20, katika mchezo dhidi ya Newcastle kutokana na utovu wa nidhamu walipokuwa katika mapumziko Dubai hivi karibuni. 

4. Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, amesema kuwa anajisikia fahari kuhusishwa na klabu ya Liverpoollakini anahisi kuwa huenda hayupo tayari kujiunga na klabu hiyo ambayo anasema ni "timu nzuri zaidi duniani."

5. Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amesisitiza kuwa atacheza kwa moyo wote kwa Chelsea licha ya kushindwa kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi uliopita.


EmoticonEmoticon