Habari 5 Kubwa Za Soka Ijumaa Feb 21

1.Wachezaji wa Atletico Madrid walishikwa na hasira na kushangazwa baada ya kukosolewa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp. Atletico iliwafunga Liverpool 1-0 Jumanne katika raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, wachezaji wa Atletico wanamtaka Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa.

2. Manchester City na Barcelona wanaminyana kumsajili beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, na klabu itakayofanikiwa kumnyakua itabidi itoe dau la zaidi ya pauni milioni 75.

3. Klabu za Juventus na Inter Milan wanavutiwa kumsajili beki wa pembeni wa Chelsea Emerson Palmieri, 25, lakini bado ofa rasmi hazijatumwa ajenti wake abainisha.

4. Arsenal wanapanga kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah ambaye kwa mujibu wa mkataba wake anathamani ya pauni milioni 34.

5. Klabu ya Inter Milan inajipanga kutoa wachezaji kwenda klabu ya Verona kama sehemu ya mpango wa kumnasa beki wa Albania Marash Kumbulla, 20, ambaye pia anawaniwa na Liverpool


EmoticonEmoticon