Habari 5 Kubwa Za Soka Jumanne Feb 18

1.Tottenham na Everton wanamuwania beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye anachezea kwa mkopo na klabu Roma.

2. Winga Raheem Sterling, 25, ataendelea kusalia Manchester City licha ya klabu hiyo kupigwa marufuku kushiriki michuano ya Ulaya, amedai wakala wake.

3. Barcelona wanatarajiwa kufanya usajili wa dharura kwa kumnyakua mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough Martin Braithwaite, 28, kutoka klabu ya Leganes.

4. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yungali anavutiwa na mshambuliaji wa Kijerumani Timo Werner, 23, lakini bado klabu ya Liverpool haijaabzisha mazungumzo na RB Leipzig juu ya usajili wa nyota huyo.

5. Kiungo Mfaransa Matteo Guendouzi, 20, anakabiliwa na mapambano ya kusalia katika klabu ya Arsenal baaada ya kuachwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Newcastle.


EmoticonEmoticon