Habari 5 Kubwa Za Soka Jumapili Feb 16

1.Aliyekuwa meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anaweza kuchukuwa nafasi ya kocha wa Manchester City Pep Guardiola iwapo raia huyo wa Uhispania ataamua kuondoka klabu hiyo.

2.Hatma ya maneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer iko mashakani baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji watatu waliokuwa walengwa katika kipindi cha usajili cha Januari.

3. Inter Milan itamruhusu mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kujiunga na Barcelona iwapo itafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. 

4. Liverpool ipo katika mazungumzo ya mwisho mwisho a kumsajili RB Leipzigstriker Timo Werner, ikiwa na nia ya kufikia kiasi cha £48m kwa mchezaji huyo wa Ujerumani.

5. Meneja wa Inter Milan Antonio Conte ameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30.


EmoticonEmoticon