Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano Feb 12

Jadon Sancho
1.Manchester United iko tayari kuipiku Chelsea katika kinyang'anyiro cha kutoa dau la £120m kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19.

2.Manchester United inaweza kufufua hamu yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 Moussa Dembele mwisho wa msimu huu.

3. Mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, ana uwezekano mkubwa kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu huku Chelsea, Manchester United na Arsenal zote zikipigania saini yake.

4. Liverpool inajiandaa kumpatia beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, 28, mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya £150,000 kwa wiki.

5. Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho alitazama mechi ya sare ya 0-0 ya Bayern Munich dhidi ya RB Leipzig siku ya Jumapili , huku beki wa Leipzig na Ufransa Dayot Upamecano, 21, akiwa mmoja ya wachezaji aliokua akitaka kumsajili.


EmoticonEmoticon