Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatano Feb 19

1.Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu lakini klabu hiyo inataka zaidi ya £150m kumuachilia mchezaji huyo wa miaka 26.
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola anasema kuwa ana mpango wa "kuwasiliana" na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer baada ya majibizano makali kumhusu mteja wake.
Ndugu wa Pogba wa kiume Mathias anasema kuwa "kila mtu anajua" kwamba anataka kuondoka Manchester United "kwenda kucheza soka ya Champions League na kushinda mataji".
2. Manchester United wanatafakari uwezekano wa kuwasajili mkurugenzi wa zamani wa michezo Paris St-Germain Antero Henrique na mkuu wa michezo wa Red Bull Ralf Rangnick katiki wadhifa wa mkurugenzi wa kiufundi. 
3. Barcelona inamlenga mshambuliaji wa Denmark na Leganes Martin Braithwaite, 28, baada ya kupewa ishara ya kumtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, baada ya kusitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad Mrazil Willian Jose, 28.
4. Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ataelekezewa darubini kali ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Champions League msimu huu. 
Timu hiyo pia inamtafuta kiungo wa kati wa Birmingham City mwenye umri wa miaka 16 Jude Bellingham, lakini Manchester United, Barcelona na Real Madrid pia zimeonesha nia yakumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka -17.
5. Manchester City inamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry, 24, kama sehemu ya mpango utakaomwezesha Leroy Sane, 24, kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga.
Timu hiyo huenda ikakabiliwa na uchunguzi zaidi kutoka Uefa ili kubaini kiwango cha wafadhili wake wa Abu Dhabi baaada ya kuwekewa marufuku ya kushiriki mashindano ya ulaya baada ya kupatikana na kosa la kiuka sheria ya uchezaji haki kifedha. 


EmoticonEmoticon