Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu Feb 17

Pep Guardiola


1.Pep Guardiola atasalia kuwa mkufunzi wa Manchester City hata kama klabu hiyo itashindwa kukabiliana na marufuku ya kutoshiriki Champions League kwa miaka miaka miwili .

2. Ajenti wa winga wa Manchester City Raheem Sterling amesema kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 25 amejitolea kuhudumia" klabu hiyo na kwamba "hatashawishiwa na mazungumzo yoyote ya uhamisho kutoka klabu hiyo kwa sasa".

3. Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer haamini kuwa wakishindwa kujikatia tiketi ya kushiriki Champions League kutaathiri mpango wa uhamisho wa klabu hiyo. 

Solskjaer anasema uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria wa miaka 30, Odion Ighalo kuja Manchester United kutoka Shanghai Shenhua huenda ukafanywa wa kudumu.

4. Barcelona italazimika kumjumuisha mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann katika mpango wowote utakaojaribu kuishawishi Inter Milan kuwauzia Lautaro Martinez.

5. RB Leipzig inasisistiza kuwa Liverpool haijawasiliana nayo kuhusu mshambuliaji wake Timo Werner. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 20 katika ligi kuu ya Bundesliga msimu huu.


EmoticonEmoticon