Habari 5 Kubwa Za Soka Jumatatu Feb 24

1.Barcelona wanakaribia kukamilisha mpango wa kusaini mkataba na Hugo Guillamon, maarufu kwa kwa pasi za guu lake la kushoto ambaye anacheza safu ya kati-nyuma mwenye umri w amiaka 20, katika timu ya wachezaji wa akiba ya Valencia ya Mestalla.

2. Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa klabu wa AC Milan Paolo Maldini anasema Mswidi Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 38, amefanya marekebisho ya kipengele cha mkataba wake iwapo Wataliano watafuzu kuingia Klabu Bingwa Ulaya.

3. Aston Villa na West Ham kwa pamoja zinamfuatilia kwa karibu mchezaji aliyethamanishwa kwa viwango vya juu wa klabu ya Gillingham Muingereza Jack Tucker mwenye umri wa miaka 20 anayecheza safu ya kati ya ulinzi.

4. Meneja wa Roma Paulo Fonseca anataka kusaini mkataba na wachezaji Chris Smalling, wa Manchester United mwenye umri wa miaka 30- ambaye pia ni mlinzi wa England, na kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 31, kwa mikataba ya kudumu.

5. Kocha wa Paris St-Germain Thomas Tuchel anaaminiwa kuwa katika maungumzo na Bayern Munich juu ya uhamisho wa kumrejesha katika nchi yake ya asili ya Ujerumani.


EmoticonEmoticon