Idadi Ya Wanaotaka Kuuaga Mwili Wa Kobe Bryant Imekuwa Tofauti Na Ilivyotegemewa

Ukumbi maarufu wa Staples Center uliopo mjini Los Angeles unaingiza watu 20,000 pekee, ukumbi huo ndio ambao utatumika leo kwa ajili ya zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kobe Bryant na binti yake Gianna.

Hata hivyo meelezwa kuwa watu 88,000 wametuma maombi ya kupata tiketi ikiwa ni ndani ya masaa 5 tu, idadi ambayo inakinzana na uwezo wa ukumbi huo maarufu. Kwa mujibu wa TMZ.

Staples Center ndio ukumbi ambao ulitumika pia kuwaaga mastaa kama Michael Jackson, Nipsey Hussle na wengine.


EmoticonEmoticon