Jack Chan Kutoa Donge Nono Kwa Mgunduzi Wa Kinga Ya Virusi Vya Corona

Jackie Chan
Mkongwe wa filamu nchini China Jackie Chan ametangaza rasmi kupitia mtandao wa Weibo kuwa atatoa fedha kwa ajili ya mtu yoyote atakayegundua kinga ya ugonjwa wa corona.
Chan ameweka wazi kiu yake ya kutaka kumaliza kabisa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Corona kwa kutangaza kutoa Zaidi ya dola za kimarekani 140000 kwa mtu ama kikundi kitakacho fanikisha kugundua kinga dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Idadi ya watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vipya vya Corona imeongezeka na kufikia 1000 na tayari shirika la afya duniani WHO limeutangaza ugonjwa huo kuwa janga la kimataifa.


EmoticonEmoticon