Jay-Z Atolea Ufafanuzi Swala La Kukaa Chini Yeye Na Mke Wake Wakati Wimbo Wa Taifa Ukiimbwa

Baada ya kutokea kwa sintofahamu juu ya The Carter's (Jay-Z, Beyonce na Blue Ivy) huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kuponda kuhusiana na watatu hao kubaki wamekaa kwenye viti vyao wakati wimbo wa taifa la Marekani ukiimbwa kwenye ufunguzi wa fainali za Super Bowl 2020.

Kwa mujibu wa Page Six, maswali mengi yaliibuka kwamba kwanini Jay-Z alibaki amekaa wakati aliwahi kusema hata kuja kufanya hivyo? Hata hivyo Jay-Z amefunguka juu ya hilo baada ya kuulizwa alipokitembelea Chuo cha Columbia Jumanne hii.
Jay-Z alijibu kwa kukataa kwamba hakuwa amekaa, alibaki amekaa mara baada ya Beyonce kumwambia kitu kuhusu muimbaji (Demi Lovato) ambaye alianza kwa kusuasua sekunde za mwanzo katika kuimba wimbo wa taifa
.
"Beyonce alikuwa ananielekeza kitu kwenye uimbaji wa Demi Lovato, ni kwa sababu yeye ana uzoefu kutokana na kuwahi kutumbuiza kwenye fainali hizo"


EmoticonEmoticon